Niliapa ukiondoka mpenzi, ntaondoka nawe
sikuahidi kukufuta machozi, bali ntalia nawe
Ina maana hata kuondoka mpenzi hukunitazama, hutaki Awena,
 basi kama nna kosa kwako nililofanya nieleze awena
Chozi langu la thamani unaliacha lianguke eeh,
tulopanga zamani ina maana si chochote
Utamu wa mapenzi niujuao mi nawe, kipenzi changu awena
utamu wa mapenzi niujuao mi nawe rudisha moyo awenaa
Iweje penzi langu kwako umelikatisha iwejee
Iweje penzi langu kwako umelikatisha ina maana tunda langu basi utamu umekwisha babyyyyy

By: Kassim Mganga
Song: Awena

Comments